Frequently
asked questions

Can't find your answer? We're here to help! Ask one of our advisors at [email protected]

Branch hurahisisha mtu yeyote kupata mkopo nchini Tanzania, wakati wowote, popote. Kamilisha fomu yetu ya maombi ndani ya sekunde, na upate mkopo wako moja kwa moja kwenye akaunti yako ya simu. Ichukulie Branch kama tawi la benki kwenye mfuko wako. Ipo kwa ajili yako wakati wote. Tembelea tovuti yetu tovuti kujifunza zaidi.
Branch ina ofisi jijini Nairobi, Kenya; Lagos, Nigeria; Mji wa Mexico, Mexico; Mumbai, India; na San Francisco, Marekani.
Kwa sasa, Branch inafanya kazi nchini Kenya, Mexico, India, Tanzania na Nigeria.
Ndio! Tafadhali hakikisha unatumia toleo la hivi karibuni la programu. Baada ya hapo, katika programu yako nenda kwenye “Akaunti Yangu”, kisha bonyeza “Mipangilio ya Programu”, halafu chagua “Lugha” kisha chagua “Kiswahili” na ubonyeze “Wasilisha” ili kuhifadhi mabadiliko.
Unaweza kufuata kiungo hiki na ubonyeze Sasisha. Au unaweza kwenda Google Play, tafuta "Branch International" kisha bonyeza "Sasisha".
Nchini Tanzania, sisi tunakubali Vodacom na Tigo. Ni matumaini yetu kukubali mitandao zingine hivi karibuni.
Asante kwa kutaka kujiunga! Tafadhali fuata hii kiungo kuenda kwa kurasa letu la nafasi za kazi kuona orodha ya nafasi za kazi zetu ya sasa.
.Kwa sasa, tunawahimiza wateja watutumie ujumbe kupitia programu wakati wowote na tutakusaidia kutatua suala lolote ambalo unaweza kuwa nalo,Nambari yetu ya huduma kwa wateja ni +255 675 031 791. Kabla ya kutembelea ofisi, tafadhali wasiliana na mwakilishi wetu wa huduma kwa wateja ili tukusaidie kuratibu ziara yako. Ofisi yetu iko 1st Floor, Oyster Pearl Galleria, Chole Road, Oysterbay, Masaki, Dar-es-salaam.
Ili kuhariri maelezo yako ya kibinafsi, bonyeza kiungo hiki “Akaunti Yangu”, au bonyeza aikoni ya picha ya mtu kwenye kona ya juu kulia katika skrini yako itakayokupeleka kwenye “Akaunti Yangu”. Kisha bonyeza “Profaili” ili kusasisha maelezo yako ya kibinafsi.
Kusajili namba mpya ya akaunti ya fedha, bonyeza kiungo hiki kisha bonyeza "Ongeza Akaunti".
Branch hukuuliza kuthibitisha akaunti yako ya fedha ili kuhakikisha kuwa ni ya Huduma tunayoikubali na kwamba ni yako. Bonyeza kwenye kiungo hiki, kisha bonyeza namba ya simu ambayo imeandikwa HAIJATHIBITISHWA kama unataka kutumia kama nambari yako ya simu katika Branch.
Bofya "Halalisha" na kisha "Endelea". Utapokea ujumbe wa SMS kwa msimbo wa nambari 4 ambayo utaweka katika programu kuhalalisha hiyo nambari.
Unaupokea ujumbe huo kwa sababu mfumo wetu hauwezi kuisoma SIM inayotakikana katika simu yako. Tafadhali toa SIM zote zingine kutoka simu yako kisha uhakikishe kuwa SIM yako ya Vodacom, Tigo aul ipo katika simu yako na urudi ndani ya app. Unastahili kuweza kuthibitisha nambari yako.
Huku Branch, sisi huendana na viwango vya juu vya uadilifu wa data. Hii ina maana kwamba huwezi kubadilisha maelezo ambayo yalitumika hapo awali katika mchakato na kufanikwa kwa mkopo wako.
Tunasikitika kwamba mambo hayakwenda vizuri wakati huu. Tafadhali tuma ujumbe kwa wahudumu wetu na ombi lako, na ufute programu. Kama ungependa kujaribu Branch tena, tuandikie na tutaweza kuwa na furaha kusaidia.
Sifa za kupata mkopo ni rahisi - Unaweza kukidhi vigezo vya mkopo kama una akaunti binafsi ya Facebook, kitambulisho cha taifa ama cha upigaji kura na nambari ya simu (Tigo au Vodacom). Pia tutaomba idhini ya kufikia data kwenye simu yako ili kujenga alama ya mkopo.
Branch hutumia data kutoka kwa simu yako, pamoja na maelezo megine ya simu kufanya uamuzi wa mkopo. Tutaunganisha maelezo hayo pamoja na historia yako ya malipo katika Branch kupata alama ya mkopo binafsi ambayo itaamua kiwango cha mkopo unachostahiki.
Kama ombi lako halitakubaliwa, usiwe na wasiwasi! Wakati mwingine inaweza kuchukua majaribio kadhaa kabla ya kupokea mkopo. Tunakuhimiza kuendelea kuhifadhi data kwenye simu yako na kutuma tena maombi baada muda uliowekwa kwenye programu yako.
Tunalenga kushughulikia mikopo yote ndani ya masaa 24. Kwa wastani tunashughulikia mikopo chini ya masaa 3, na tunatarajia kupunguza hadi dakika chache hivi.
Branch hutumia data kutoka kwa simu yako, pamoja na vyanzo vingine kufanya uamuzi wa mkopo. Kuongeza uwezo wako wa kupata mkopo, tafadhali hakikisha umehifadhi data kwenye simu yako, uwe na sifa nzuri na Wakopeshaji Wengine na ujaze sahihi maelezo ya akaunti yako.
Mara simu itakapotumika kuwasiliana na Branch, haiwezi tena kutumika na mtu mwingine. Kama utapenda kuwasiliana na Branch, tafadhali tumia simu nyingine ambayo haijatumika kuwasiliana na Branch awali.
Kuomba mkopo ni rahisi! Baada ya kupakua programu ya Branch, unachohitaji kufanya ni kujisajili. Nenda kwenye chaguo la “Mikopo” chini katika skrini ya kwanza, na ujaze maelezo yako ya kibinafsi, nambari ya simu na maelezo ya benki. Kisha utaweza kuona ofa za mkopo zinazopatikana, chagua kiwango unachotaka, na ubonyeze “uma Ombi”.
Tuna mikopo mbali mbali kama Tsh 5,000 hadi Tsh 1,000,000. Ukilipa mkopo wako kulingana na ratiba yako, kiasi cha mkopo wako kitaongezeka.
Ofa za mikopo ambazo unaweza kuona hutegemea mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na historia yako ya malipo ya Branch. Ukulipa kila awamu kwa tarehe yake, utaweza kupokea mikopo mikubwa baada ya muda. Kumbuka kuwa ongezeko la mkopo linaweza chukua muda na pia ukichelewa kulipa kiasi kinaweza punguzwa.
Kwa bahati mbaya hutaweza kupata mkopo wa kiasi cha juu. Njia ya haraka zaidi ya kuongeza kiasi cha mkopo wako ni kufanya malipo yako kulingana na ratiba yako.
Kiasi cha juu kabisa cha mkopo tunachotoa ni Tsh 1,000,000 na tunatarajia kukiongeza hapo baadaye.
Viwango vya riba vinaamuliwa na mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na historia yako ya malipo na Branch na gharama ya kukopesha kwa upande wetu. Wakopaji wanatakiwa kulipia ada zozote za miamala ya pesa kwa simu, kama vile ada za Vodacom M-Pesa au Tigo Pesa zinazohusiana na kulipa mkopo. Ada za kawaida za SMS na data kutoka kwa mtoa huduma wako wa simu zinaweza kutumika.
Ada za usindikaji hutozwa na Branch ili kulipia gharama za usimamizi kama vile kuchakata na kuthibitisha maombi ya mkopo. Ada ya usindikaji kwa kawaida ni asilimia ya kiasi cha mkopo na itaonyeshwa katika ada za mkopo kwenye app na katika makubaliano ya mkopo. Pia tunaongeza asilimia 10% ya ada hii ya usindikaji kama kodi wa ada ya usindikaji kwa sababui hii ni kodi ambao tunatozwa na mamlaka ya kodi.
Kiasi kilichotumwa ni kiasi cha mwisho kitakachowekwa kwenye akaunti yako ya kifedha (tigopesa,mpesa n.k) baada ya kukatwa ada za usindikaji na kodi yakei. Ada hizo hukusanywa mapema ili kufidia gharama zinazotokana na Branch kwa ajili ya kuchakata na kuthibitisha ombi la mkopo na endapo kushindwa kulipa mkopo.
Kiasi kilichowekwa kwenye akaunti yako ya fedha ni Kiasi kilichotumwa, ambacho huonyeshwa katika programu na makubaliano ya mkopo unapotuma maombi ya mkopo, na kiasi hiki ni chini ya Kiasi cha Mkopo kwa sababu kiasi hiki ni kiasi kinachobaki baada ya kukatwa ada za usindikaji na kodi yake inayotozwa. Ada hizo hukusanywa mapema ili kufidia gharama zinazotokana na Branch kwa ajili ya kuchakata na kuthibitisha ombi la mkopo na endapo kushindwa kulipa mkopo.
Kiwango cha mkopo hutegemea vipengele vingi. Ingawa kiasi chako hakitaongezeka mara moja, kitaongezeka kwa muda zaidi unapoendelea kufanya malipo yako yote kulingana na ratiba yako.
Kila kiasi cha mkopo huamuliwa na mifumo yetu kila wakati unapolipa kulingana na sababu kadhaa. Tunakuhimiza ufanye malipo yako kulingana na ratiba yako ili mkopo wako uongezeke.
Kufanya marejesho fuata hatua hizi:

Vodacom

1. Piga *150*00# kupata menyu ya M-Pesa
2. Halafu bonyeza 4 kufanya malipo na Vodacom M-Pesa.
3. Bonyeza 4 kuingiza Namba ya Biashara-Kampuni, ukitumia 256699 kama namba ya biashara
4. Halafu ingiza namba uliyotumia kuchukua mkopo kama namba ya kumbukumbu
5. Katika menyu zifuatazo, unaweza sasa kuingiza kiasi cha pesa
6. Namba yako ya siri
7. Halafu chagua “1” kuthibitisha muamala.

Tigo

1. Piga *150*01# kupata menyu ya Tigo Pesa
2. Halafu bonyeza 4: Kulipa bili
3. Bonyeza 3 kuingiza Namba ya Biashara-Kampuni, ukitumia 256699 kama namba ya biashara
4. Halafu ingiza namba uliyotumia kuchukua mkopo kama namba ya kumbukumbu.
5. Katika menyu zifuatazo, unaweza sasa kuingiza kiasi cha pesa
6. Namba yako ya siri
7. Halafu chagua “1” kuthibitisha muamala.

Airtel

1. Piga *150*60# kupata menyu ya Airtel
2. Halafu bonyeza 5 kulipa bili
3. Bonyeza 4 kuingiza Namba ya Biashara-Kampuni, ukitumia 256699 kama namba ya Biashara.
4. Iingiza kiasi cha pesa
5. Halafu ingiza namba uliyotumia kuchukua mkopo kama namba ya kumbukumbu.
6. Namba yako ya siri
7. Thibitisha muamala.
Tunakushauri ufanye malipo yako kama inavyoonekana kwenye "Mkopo Wangu". Kuruka marejesho yako mengine na kulipa mkopo kwenye tarehe ya mwisho kutaathiri viwango vya mikopo ya hapo baadaye.
Kuangalia historia yako ya ulipaji, bonyeza kwenye salio la mkopo wako katika skrini ya kwanza au chaguo la “Mikopo” chini katika skrini ya hiyo ya kwanza, kisha bonyeza kwenye “Ratiba ya Malipo”. Utaweza kuona kiasi kinachohitajika pamoja na tarehe ya malipo.
Ikiwa hautapokea ujumbe wa malipo yako kupokelewa na Branch baada ya masaa kadhaa, Tafadhali tutumie kwenye Pragramu, ujumbe wa uthibitisho uliopokea kwa ajili ya marejesho na namba uliyotumia kufanya marejesho kupitia "Huduma Kwa Wateja" kwenye programu. Tutafuatilia na kuhuisha akaunti yako.
Ili kukuza kiwango chako cha mkopo, tunakuhimiza ulipe mkopo wako kwa kufuata “Ratiba ya Malipo”, ambayo inapatikana kwa kubonyeza “Mikopo” chini katika skrini ya kwanza.
Kama utazidisha malipo ya mwisho ya mkopo wako, kiasi kitabaki kwenye akaunti yako na kutumika juu ya ulipaji wa mkopo wako ujao.
Kulipa kila awamu kwa tarehe inayostahili kunakuruhusu kukuza hadhi yako ya mkopo na kukuwezesha kupata viwango zaidi vya mkopo. Ucheleweshaji wa malipo utaathiri uwezo wako wa kupata mikopo inayofuata au kubwa zaidi. Ada ya kuchelewa ya % inaweza kutozwa kwa kiasi ambacho hakijalipwa kwa baadhi ya mikopo. Ukichelewa sana kufanya malipo yako, tunaweza kukuorodhesha kwa Mamlaka ya Mikopo Tanzania.
Kwa bahati mbaya hutaweza kubadilisha awamu za marejesho baada ya kupokea mkopo. Kama huna uwezo wa kukamilisha deni lote lililochelewa, tunakushauri kuanza kufanya angalau marejesho kidogo kutoka leo.
Mamlaka ya Mikopo hukusanya taarifa ya mikopo ya watu binafsi na inaweza kutoa taarifa yako ya malipo kwa mabenki, wakopeshaji, na waajiri wako. Mamlaka ya Mikopo husaidia kukuza ushirikishwaji wa fedha na kuzuia madeni zaidi.
Baada ya kulipa deni lililopitisha wakati, unaweza kutuandikia kupitia programu ya Branch, na tutakushauri zaidi.
Tunaficha taarifa unazochagua kushirikisha nasi ili kulinda faragha yako. Tunachukulia faragha yako kwa umakini mkubwa na kuahidi hatutashiriki habari zako na watu wengine bila ya ridhaa yako mahususi ila kwa shughuli kama kushirikisha maelezo juu ya mkopo ambao umekuwa batili kwa shirika kama Mamlaka ya Mikopo. Hatuuzi maelezo wala taarifa zako.
Kitambulisho chako ndicho hati pekee ambacho kinakutofautisha na mtu yeyote. Tunaelewa kuwa hii ni habari yako ya kibinafsi na tunachukua maelezo ya kibinafsi ya wateja wetu kwa umakini sana. Habari hii inatumika tu kuhakikisha kwamba akaunti ni yako, na hakuna mtu mwingine anayeweza kuomba mkopo kwa kutumia akaunti yako. Ikiwa una maswali zaidi, tafadhali wasiliana na timu ya huduma kwa wateja wa Branch.
Branch hutumia data kutoka kwa simu yako, pamoja na maelezo mengine ya simu kufanya uamuzi wa mikopo. Data hii ni sehemu muhimu sana ya kufanya maamuzi ya mchakato wetu, na inaturuhusu kutoa huduma za kifedha bora na za kiwango ya juu.
Katika simu yako ya Android, tafadhali nenda kwa Mipangilio > Programu > Branch > Ruhusa na kuhakikisha kwamba umewezesha Branch kufikia kila kitu.